MKALI wa Bongo Fleva ambaye pia ni mkali wa mavazi, Q Boy, baada ya kumuangukia aliyekuwa rafiki yake na Boss wake, Diamond Platnumz, na kumtaka wamalize tofauti zao ili waishi kwa amani amepiga stori na Global TV na kuzungumzia ndoa ya Diamond.
Q Boy amesema kama Diamond atamuoa mchumba ake wa sasa kutoka Kenya, Tanasha Donna, siku ya Valentine Februari 14, basi atafurahi sana maana siku hiyo itakuwa ni siku yake ya kuzaliwa hivyo ataungana nae katika kusheherekea harusi yao.