×

AJIB Atinga Kwenye Party ya MANARA / Anunua Pafyumu kwa Laki 5 – video

NAHODHA wa Yanga Ibrahim Ajibu amemsapoti msemaji wa Simba Haji Manara katika uzinduzi wa Pafyum yake na Haji Manara Foundation ambayo imefanyika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam huku ikikutanisha mastaa kibao.

Ajibu amechangia kwa kununua pafyum ya DE LA BOSS kwa shilingi laki tano kama mchango wake katika hafla hiyo pamoja na Foundation ya Manara.

Hata hivyo Ajibu amekataa kuzungumzia mechi ya fainali ya Sportpesa Cup ambayo Sharks Karioabng ameibuka na ushindi na kubeba kombe hilo mechi ilichezwa jana uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club