×

TEDEF WAONGOZA KONGAMANO LA KUMPONGEZA MAGUFULI

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Economic Diplomacy Elevation Foundation (TEDEF) waandaaji wa kongamano la kumpongeza Rais John Magufuli,  akizungumza wakati wa ufunguzi.

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Tanzania Ecomic Diplomacy Elevation Foundation (TEDEF)  kwa kushirikiana na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali, juzi (Jumamosi) lilimpongeza Rais  John Magufuli kwa kasi ya juhudi zake  kuleta maendeleo nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa TEDEF, Telesphory Kyaruzi na wadau hao wa maendeleo, walitoa pongezi hizo kwenye kongamano lililofanyika Ukumbi wa Meya wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar ambapo mgeni maalum alikuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Kate Kamba,  aliyemwakilisha Katibu Mwenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria, Profesa Deus Ngaruko, akitoa pongezi kwa rais alivyofanikisha mambo makubwa kwa kipindi kifupi alichokaa madarakani.

Miongoni mwa mambo aliyopongezwa JPM ni kufanikisha mradi wa umeme wa Stigler’s Gorge, ujenzi wa reli yenye uwezo mkubwa (Standard Gauge) na miundo mbinu mbalimbali zikiwemo barabara,  jambo ambalo ndiyo chanzo kikuu cha kukua kwa uchumi.

Matukio katika picha:

Washiriki wakiwa kwenye umakini wa kusikiliza.
Mgeni rasmi, Kate Kamba,  akiandika mambo muhimu yaliyokuwa yakizungumzwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Diplomasia kutoka Chuo cha Diplomasia, Dkt. Burhani Mtengwa,  akielezea jinsi  JPM alivyofanikisha diplomasia ya kiuchumi na kuleta maendeleo ya kasi ya kiuchumi.
Mwenyekiti wa Muungano wa Vicoba (VIGUTA), Salmini Daudi, akielezea jinsi alivyofanikiwa kuanzisha benki ya vijana hapa nchini kutokana na maendeleo ya kiuchumi yaliyoletwa na uongozi wa sasa. Salmini alisema benki hiyo itawawezesha vijana kupata mitaji ya kujikwamua kimaisha.
Mkurugenzi wa VHIF, Peter Mayunga,  akimpongeza serikali ya JPM kwa mkakati wake wa kuimarisha mradi wa umeme na kueleza jinsi umeme utakavyoweza kurahisisha maisha ya majumbani, viwandani, mashambani na sehemu nyingine,  hivyo  kuvuta wawekezaji zaidi.
Mkuu wa mkoa mstaafu, Dkt. Ibrahim Msengi,  naye akielezea mafanikio ya kimaendelea ndani ya kipindi kifupi cha awamu ya sasa.
Mmoja wa wajumbe  akitoa maoni.
Dkt. Kyaruzi (kulia) na Mutabuzi wakimpa Kate Kamba, cheti maalum cha heshima na kutambua yaliyofanywa na Rais Magufuli katika kipindi kifupi.

 

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL