×

Zahera: Sasa Tupo Safi Kila Idara

KOCHA mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefungukia furaha aliyonayo baada ya wachezaji wake waliokuwa wanasumbuliwa na majeraha kuwa fiti.

 

Yanga ilikuwa inakabiliwa na majeruhi wengi kwenye kikosi chake hali iliyopelekea ufinyu wa kufanya mabadiliko ya wachezaji kwenye baadhi ya mechi zake.

 

Papy Tshishimbi, Ramadhan Kabwili, Raphael Daud, Juma Mahadhi na Thaban Kamusoko ni baadhi ya nyota ambao walikuwa nje ya kikosi kwa muda mrefu wakiuguza majeraha.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Zahera alisema kuwa anafurahi kuona wachezaji wake wamerejea kikosini, hali ambayo itaongeza nguvu zaidi kwenye timu kuelekea michezo ya ligi na mchezo wa kesho wa Kombe la FA dhidi ya Biashara.

 

“Nafurahi sasa timu itacheza ikiwa haina mchezaji yeyote ambaye atakuwa na majeraha, wale wote ambao walikuwa nje wamerejea kikosini.

 

“Yanga itakuwa inacheza mechi ikiwa na wachezaji wake wote, kwa sababu wale walikuwa nje wakiuguza majeraha tayari wamepona, nafikiri ni jambo jema kuelekea mchezo wetu na Biashara,” alisema Zahera

Issa Liponda