×

Tatu Mzuka Yaja na Siku 28 Kwa Wapendanao (Picha + Video)

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Sebastian Maganga, akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu kampeni ya Siku 28 za Valentino iliyoanzishwa na kampuni ya Network.

KAMPUNI the Network inayoratibu mchezo wa Tatu Mzuka leo imetambulisha kampeni yake mpya inayokwenda kwa jina la Siku 28 za Valentine ambapo kwa wapendano wawili mkicheza na mmoja wenu akishinda maana yake mtakuwa mmeshinda wote fedha  itakayowawezesha kula bata siku hiyo ya Wapendanao.

…Akifafanua jambo.

Akizungumza mapema leo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Sebastian Maganga, amesema, kila siku wapendanao watapata fursa ya kushinda Sh. milioni 2 (yaani milioni 1 kwa mshindi na milioni 1 kwa ampendaye) huku wapendanao watano na wawapendao wakishinda mamilioni kila usiku wa Jackpot.

“Unaweza kuupeleka upendo wako katika kiwango kingine kwa kucheza shilingi 500 kwenda namba ya kampuni ambayo ni 55511.  Anza kucheza sasa, kabla watu wengi hawajashtukia,  Wewe na mpenzi wako mnaweza kushinda Milioni 2. Ila hakikisheni mnaandika neno WEB baada ya namba zenu za bahati,” alisema Maganga.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club