KESHO BONGE LA COMEDY, NYERERE, JK, MC PILIPILI, BLACK PASS NDANI
Kiongozi wa Kundi la Chekelea Stand Up Comedy, Oscar Luambano a.k.a Oscar Nyerere akizungumza na wanahabari kwenye Hoteli ya Kebbys iliyopo Mwenge jijini Dar, amesema kundi hilo kesho linatarajia kufanya tamasha kubwa kwenye ukumbi wa hoteli hiyo.
Oscar amewataja baadhi ya wachekeshaji wenzake atakaokuwa nao katika tamasha hilo kuwa ni pamoja na MC Pilipili, Dogo Pepe, Back Pass, JK Comedian na wengineo.
Katika tamasha hilo, mgenio Rasmi anatarajiwa kuwa ni Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michgezo, Juliana Shonza huku waimbaji wa Injili akiwemo Emmanuel Mbasha na mastaa wengine wa filamu wakitarajiwa kutinga ndani.
HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL
Comments are closed.