The House of Favourite Newspapers

Bocco Amjaza Mkwanja shabiki

Mshambuliaji wa Simba, John Bocco

PASI aliyoitoa mshambuliaji wa Simba, John Bocco kwa Meddie Kagere wakati walipocheza na Waarabu Al Ahly, jana Alhamisi ilimnufaisha shabiki wa Simba baada ya kushinda kiasi cha Sh 26,000 ikiwa ni kutokana na kuibuka kwa mvutano baina yake na shabiki mwenzake.

 

Shabiki huyo, Pe­ter Mussa alijipatia kiasi hicho kwenye mazoezi ya Simba, jana kwenye Uwan­ja wa Boko ikiwa ni baada ya kum­shinda mwenzake ambaye waliweka dau la kiasi cha Sh 13,000 baada ya kuzuka kwa ubishani juu ya pasi ya Bocco kwenda kwa Kagere alitoa kwa kichwa au kifua.

 

Mashabiki hao walianza ku­bishana kwa muda mrefu juu ya pasi aliyoitoa Bocco kwenye mechi ya Al Ahly wakati wa mazoezi ya timu hiyo yakien­delea kabla ya mwisho ubis­hani wao kumalizwa na Bocco mwenyewe.

 

Baada ya mazoezi kumalizika Bocco al­iulizwa na mashabiki hao wakitaka kujua ni namna gani alivyotoa pasi hiyo kabla ya kujibu aliitoa kwa kichwa na kumfanya shabiki huyo ajipatie kiasi hicho cha Sh 26,000 lakini akaamua kutoa Sh 5,000 akampa Bocco kama zawadi kwa kumaliza ubishi.

Comments are closed.