The House of Favourite Newspapers

UWOYA:USITHUBUTU KUOLEWA NA USIYEMPENDA

Irene Uwoya

STAA wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya ameibuka na kuwaasa wanawake kuwa kamwe wasikurupuke kuolewa na wanaume kama moyo wao haujapenda kweli. Akizungumza na Risasi Jumamosi, Uwoya alisema hiyo imewahi kumtokea akaolewa na mwanaume ambaye hakumpenda kitu ambacho kilimtesa hivyo wanawake wasiolewe ili tu waonekane nao wameolewa bali waingie kwenye ndoa na watu ambao wamewapenda kwa dhati.

“Jamani wanawake wenzangu hakuna kitu kinachotesa kama kuolewa na mwanaume ambaye moyoni mwako hayupo, ni mateso makubwa hiyo ilishanitokea kwa hiyo nawasihi msijaribu kufanya hivyo kwani naamini ukitaka kuifurahia ndoa ni kuolewa na mwanaume unayempenda,” alisema Uwoya bila kumtaja jina mwanaume huyo. Hata hivyo, inafahamika kuwa, Uwoya amewahi kuingia kwenye ndoa na mcheza soka wa Rwanda, marehemu Hamad Ndikumana ‘Ndiku’ na bwa’mdogo kutoka Bongo Flevani, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’.

STORI: Imelda Mtema

Comments are closed.