
KAMANDA wa Polisi Kinondoni, Mussa Taibu amesema msanii, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’ anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Polisi Oyster Bay jijini Dar es Salaam kwa mahojiano kutokana na tuhuma za kukashifu na kutoa lugha za kejeli kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, marehemu Ruge Mutahaba.
Jana Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe alilielekeza Baraza la Sanaa Taifa (Basata) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kumchukulia hatua ‘Dudu Baya’ kwa kumdhihaki Ruge ambaye alifariki jana nchini Afrika Kusini.
Lakini baadaye kupitia akaunti yake ya Instagram, Dudu Baya alimjibu waziri huyo na kusema asisumbuke kuwaagiza polisi wamsake kwani watapoteza mafuta bure, badala yake wamuelekeze ni kituo gani cha polisi akaripoti.
MWAKYEMBE Amvaa DUDU BAYA “Ni Mpuuzi, Rais Ameshtuka, Akamatwe Haraka”
“Nipo nyumbani, Mheshimiwa Mwakyembe umeagiza polisi kunitafuta, usisumbue difenda kumaliza mafuta, bora wakakamte majambazi, niambie polisi waniite kituo gani, nipo tayari kufika hapo,”amesema Dudu Baya.
Tukio hilo limewafanya watu wengi ambao kwa sasa wapo kwenye majonzi, kuchukizwa na kitendo hicho cha kumdhihaki marehemu kwenye mitandao ya kijamii badala ya kumwombea pumziko la amani.
Imedaiwa kwamba kupitia mitandao ya kijamii msanii huyo amekuwa akitumia maneno ya kuandika, kujirekodi video na kuzisambaza akimkejeli marehemu Ruge.
Maneno Mazito ya WAZIRI MKUU Msibani kwa RUGE, Yatakutoa Machozi!