×

ETI TESSY KAMDILITI KABISA ASLAY

BAADA ya miezi kadhaa kupita tangu Aslay amwagane na mzazi mwenzake ,Tessy, hati­mae mwanadada huyo amefunguka.

 

Amedai kwamba kwa sasa hapotezi muda wake kumu­waza mwanaume huyo, kwani ame­shamsahau na sasa ana maisha yake mengine.

 

Akizungum­za na Spoti Xtra, Tessy alisema kuwa alipata shida mwanzoni lakini tangu agundue kwamba msanii huyo hakuwa chaguo lake alia­mua kuishi maisha yake.

“Nilipata shida sana mwanzo­ni, kila mtu alikuwa ananishauri anavyojua yeye, lakini nashuku­ru Mungu siku zilienda na sasa hivi nimesham­sahau kabisa.

 

“Kilichobaki kati yetu ni kumlea tu binti yetu Moza basi, pia sidhani kama naweza nikarudi tena kwake nina maisha yangu na ninayafu­rahia,” alisema Tessy