Kauli ya kwamba marehemu, Ruge Mutahaba alikuwa kipenzi cha watu imezidi kujidhihirisha zaidi kwenye msiba wake kwani watu kutoka maeneo mbalimbali wameweza kufunga safari hadi mkoani Kagera kwa ajili ya kumzika akiwemo, Sister K, ambaye amefunga safari kutoka mkoani Njombe.
Sister K amesema kitu kilichomsukuma zaidi kutoka Njombe hadi Kagera ni kutokana na jinsi ambavyo Ruge alimpokea kwa upendo alipoingia katika Jumba la Vipaji (THT) akiwa msanii na fundi wa kupiga gitaa.
Comments are closed.