Mkurugenzi Mtendaji wa NBC amtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Global Publishers March 6, 2019
SHARE THIS:
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Theobald Sabi (kulia), wakati mkurugenzi huyo akimtembelea ofisini kwake Ilala, Dar es Salaam hivi karibuni Kushoto ni Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe. Mazungumzo yao yalijikita katika kuangalia namna mbalimbali za kudumisha ushirikiano wa pande zote mbili.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Theobald Sabi (kulia) pamoja na Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe, alipotembelewa na viongozi hao wa NBC ofisini kwake Ilala, Dar es Salaam hivi karibuni.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Theobald Sabi (kulia) pamoja na Meneja Mahusiano wa NBC William Kallaghe.