
WAZEE wa mikeka kwenye maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam jana walikiri kweli Gazeti jipya la bure la Betika siyo mchezo.
Mikeka kibao waliotandaza kwa kufuata maelekezo ya Betika ambalo linapatika bure mitaani imetiki. Toleo la jana Jumatano ambalo mpaka leo linapatikana kwenye baadhi ya meza za magazeti, lilitimiza mwezi mmoja tangu liingie mtaani.

Gazeti hilo hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 na huwa linatoka kila Jumatano likiwa na mikeka kibao ambayo wazee wa kubeti wamekubali kwamba ndiyo yenyewe.
Kila likitoka, maofisa masoko wa Kampuni ya Global Publishers ambayo ndiyo inachapisha gazeti hilo, huingia mtaani kupata maoni ya wasomaji ambapo wengi wameonekana kulimwagia sifa na kusema hawajawahi kuona kitu kizuri kama hicho kwenye ishu za kubeti kwani sasa kazi yao imekuwa rahisi hawaumizi kichwa.
Jana maeneo ya Msimbazi Center, Ilala, Buguruni, Tandika,Temeke, Mbagala na Mwenge mpaka Kigamboni mambo yalikuwa ni shangwe na usiku wa kuamkia leo mdosi kagaragazwa kwelikweli na wazee wa kubeti.
“Gazeti hili ni zuri, ukilisoma hata kama hauna mpango wa kubeti basi lazima ubeti kwa sababu linakupa njia nzuri ya kushinda na mara kadhaa watu wanashinda kutokana na mbinu zilizopo humu ndani,” alisema mmoja wa wasomaji maeneo ya Mbagala.
Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, alisema kuwa mapokea ya gazeti hilo kila siku yanazidi kuwa juu hali inayodhihirisha kwamba wasomaji hasa wazee wa kubeti walikuwa na kiu kubwa ya bidhaa kama hiyo.
“Tangu liingie mtaani, tumepata mrejesho mzuri kwamba wasomaji wanalihitaji sana, hivyo tutaendelea kuwapa vitu vizuri wasomaji wetu ili kukata kiu yao.
“Lakini ukingalia toleo la leo (jana), lina mambo mengi yanayohusu michezo ya kimataifa kama mechi ya Man U na PSG, hivyo watu wa kubeti wanapata maujanja ya kubashiri mchezo huo na kushinda,” alisema Mgema. Gazeti hilo lenye kurasa 20 ambazo zote ni za rangi, mbali na kuwa na makala na odds za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi kubwa barani Ulaya.