
KATIKA kuhakikisha inapata ushindi kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Samora dhidi ya Yanga leo, uongozi wa Lipuli FC, umesema umetenga Sh mil 3 kama motisha kwa wachezaji wao ikiwa watashinda mchezo huo.
Lipuli ambayo ina pointi 41 katika nafasi ya sita, leo itakuwa nyumbani ikisaka pointi 3 muhimu mbele ya Yanga ambayo ipo kileleni na alama zake 67 baada ya kucheza mechi 27.

Mara ya mwisho timu hizo kukutana Yanga ilishinda 2-0 Uwanja wa Samora. Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdalah, ndiye aliyetoa fedha hizo ili kuhakikisha Lipuli inapambana na kushinda mechi hiyo.
Msemaji wa Lipuli, Festo Sanga ameliambia Championi Jumamosi kuwa: “Tumepokea milioni tatu na katoni za maji kutoka kwa DC wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdalah, kwa lengo la kuwapa motisha wachezaji ili waweze kuifunga Yanga kwenye mchezo wa leo.”
Issa Liponda, Dar es Salaam