JIDE, MAI MARTHA WACHONGANISHWA
MWANAMUZIKI Judith Wambura ‘Jide’ na mtangazaji Maimartha Jesse ‘Mai’ juzikati walichonganishwa baada ya mashabiki kudai kuwa, eti Mai ni mnafiki kwa kuwa kipindi cha msiba wa bosi wa Clouds, Ruge Mutahaba alimnanga mwenziye kwa kutohudhuria msiba wake kisha baadaye kuanza kumsifia.
Sakata hilo lilianza hivi; juzikati Maimartha alikomenti kwenye peji ya Insta ya Jide akimsifia, kitendo ambacho kilionesha kuwakera wafuasi wa Jide ambao walimwita Mai mnafiki na kumtaka Jide ‘amblok’
Baada ya baadhi ya mashabiki kushadadia hilo, Jide alikomenti kuwa hata watu wanafiki yeye anawablok kwani hajali; akaandika; ‘I don’t care’ maneno yaliyobeba jina la wimbo wake mpya.
Mwandishi wetu hakuweza kumpata Jide kuzungumzia ishu hiyo lakini Mai alipopigiwa simu na kuulizwa anachukuliaje hilo la kuitwa mnafiki alisema: “Namheshimu Jide, ni dada yangu kabisa wakati mwingine ni hizi kazi tu, wala siwezi kugombana na Jide kabisa, wanaotuchonganisha wanafanya vibaya sana.”
Comments are closed.