×

BREAKING: NYIKA, LUKUMAY WAACHIA NGAZI YANGA

 

Hussein Nyika (kushoto) na Samuel Lukumay wakizungumza mbele ya waandishi wa habari makao makuu ya Klabu ya Yanga, Kariakoo, Dar es Salaam, leo.

KAIMU Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, Samuel Lukumay,  na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika,  wametangaza kujiuzulu nafasi zao.

 

Wawili hao wameamua kuachia ngazi mapema ili kupisha mchakato wa uchaguzi mkuu wa klabu ambao utakaofanyika hivi karibuni.

 

Pamojana kujiuzulu, Nyika amewaomba msamaha  wote aliowakosea pindi akiwa madarakani katika  klabu hiyo.

 

”Ninajiuzulu nafasi zangu zote nikiwa mjumbe wa kamati ya utendaji.  Lakini pia nikiwa mwenyekiti wa kamati ya usajili na kamati ya mashindano,  na niombe msamaha kwa wale niliowakosea katika utekelezaji wangu wa majukumu,” alisema’.

 

Hivi karibuni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Yanga, George Mkuchika, alitangaza kuwa watakuwa na mkutano mkuu maalum utakaoamua kama klabu inahitaji kufanya uchaguzi mkuu ama la wa kujaza nafasi  zilizo wazi.

 

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika siku za usoni ili kufikia mwafaka  ili kufanya uchaguzi mkuu mwaka huu  ili kutoingiliana mwakani na uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani nchini.