×

SIMBA YABANWA NYUMBANI NA TP MAZEMBE, YATOKA SARE TAIFA (PICHA +VIDEO)

Kikosi cha timu ya TP Mazembe kilichoanza dhidi ya Simba leo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

SIMBA  leo wamelazimisha sare kwenye mchezo wao wa kwanza wa hatua ya robo fainali wakiwa nyumbani mbele ya TP Mazembe kwa kutoka suluhu bila kufungana katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kiungo wa Clatous Chota Chama akiwatoka wachezaji wa TP Mazembe.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ametuma ujumbe kwa mashabiki wa Simba kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuandika ujumbe uliosomeka namna hii:-

Kiungo wa Simba Jonas Mkunde (kulia) akimkaba mchezaji wa TP Mazembe.

“Alhamdulillah,jitihada hazizidi kudra ila tuendelee kushikamana ktk Dakika tisini za Jasho na Damu kule Congo!!,” amesema Manara.

Kikosi cha timu ya Simba kilichoanza dhidi ya TP Mazembe.

Simba watarudiana na TP Mazembe ugenini ambapo ili apenye sasa anatakiwa akashinde ugenini akipigwa safari inaishia Congo, ngoma ikiwa droo mshindi anatafutwa kwa njia ya penalti.

…Makapteni wakiwa na marefa waliochezesha mchezo wa leo.