The House of Favourite Newspapers

ASLAY: NASHUKA NA BENDI DAR LIVE PASAKA HII

Aslay Isihaka

K WA mara ya kwanza tangu atoke Yamoto Band, staa wa muziki wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka amesema kuwa atashuka Sikukuu ya Pasaka (Aprili 21, mwaka huu) ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar na bendi mpya ambayo itakuwa ikipiga muziki wake live kwa kutumia vyombo.  Akizungumza na Risasi Vibes, Aslay alisema kuwa, zipo zawadi nyingi amewatayarishia mashabiki wake kwa hiyo waje kwa wingi kujionea.

“Mashabiki wote mnajua linapokuja suala la shoo huwa silembi, nitakamua live kwa kutumia vyombo hakuna cha ‘playback’ mwanzo mwisho ni burudani tu,” alisema Aslay. Naye Meneja wa Dar Live, Rajabu Mteta ‘KP Mjomba’ alisema kuwa, kwa mara ya kwanza tangu Aslay afanye muziki kivyake hajawahi kushuka katika uwanja huo wa taifa wa burudani.

“Siyo Dar Live tu, Aslay hajawahi kufanya shoo yoyote si Temeke wala Mbagala kwa hiyo kwa mara ya kwanza atashuka Dar Live Pasaka hii na kuporomosha vibao vyake kibao kuanzia Hauna, Natamba, Totoa, Nibebe, Likizo na Kwatu hivyo niwaombe mashabiki wote mjitokeze kwa wingi kushuhudia shoo hii ya kihistoria,” alisema KP na kuongeza kuwa listi kamili ya watakaosindikizwa itatajwa hapo baadaye. Burudani hiyo ya kijanja itakuwa kwa mchongo wa buku 10 tu yaani 10,000 na 8,000 kwa watu 100 wa kwanza.

Comments are closed.