
NAJUA ulisinzia au pengine hukuangalia kabisa au uliona matokeo tu kwenye livescore. Au kwenye Whatsap kwenye lile kundi la Friends of Spoti Xtra. Usiku wa leo Manchester United akiwa nyumbani alikiona cha moto kwa Barcelona.
Nilikuwa hapa Old Trafford naangalia mpira usiku wa kuamkia leo Alhamisi, nilipoangalia hali halisi ya uwanjani kwa maana ya kiwango pamoja na nyuso za mashabiki wa Manchester United nikamkumbuka Haji Manara wa Simba.

Manara wakati zinaanza kampeni za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika alitamba kwamba Simba pale Taifa hata ikija Barcelona ‘tena ile yenyewe inakula nyingi’. Achana na hii ya jana ambayo iliwatoa jasho Man United.
Katika mechi ya jana kipindi cha kwanza Barcelona walionekana kutawala kuanzia kwenye umiliki wa mpira na mbinu, jambo ambalo liliwapa goli la mapema licha ya kwamba mashabiki walionekana kushangilia mwanzo mwisho. Juhudi za Luis Suarez ziliipa Barcelona bao la kuongoza dakika ya 12 ingawa lilikuwa ni bao lililomaliziwa kimiani na Luke Shaw. Mwamuzi alidai wameotea lakini baada ya kuangalia kwenye VAR akasema mpira uende kati. Kilichotokea kipindi cha kwanza ni kwamba Barcelona waliongoza kumiliki mpira kwa asilimia 68 kwa 32 za wenyeji.

Mashuti langoni wenyeji walipiga matano kipindi cha kwanza huku Barcelona wakipata matatu. Hapo kwenye pasi sasa Spoti Xtra ambalo linatoka kila Alhamisi na Jumapili lilihesabu pasi 375 kwa Barcelona kipindi hicho na United 178. Lakini kwenye ubora wa pasi Barca walikuwa na asilimia 90 dhidi ya 84 za United.

Ni dakika 45 ambazo kijasho kiwatoka United licha ya kosakosa za hapa na pale ambazo hazikuwa na madhara sana kama za Barca. Kipindi Man United walirudi mchezoni kwa kuwabana vilivyo Barca lakini jitihada zao hazikuwa na faida kwani hadi mwamuzi anamaliza walizama kwa bao 1-0. RONALDO NA JUVE Kwenye mechi nyingine, Juve ikiwa ugenini mbele ya Ajax ilifungana bao 1-1 huku staa wa Juve, Cristiano Ronaldo akitupia
STORI NA SALEH ALLY, Manchester
MARUDIANO Barcelona vs United Siku: Jumanne Ijayo Muda: Saa 4.00 usiku
dakika ya 45 na David Neres akiisawazishia Ajax dakika ya 46.