
MOTO ambao wanaenda nao Yanga siyo wa nchi hii kwani jana Alhamisi waliendelea kuwaacha mbali wapinzani wao, Simba kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara kutokana na kupata ushindi.
Yanga walicheza pambano lao la 31 la ligi msimu huu ambapo walishinda kwa mabao 3-2 katika mechi ngumu mbele ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba ambapo wameweka makazi yao ya muda mfupi.
Kwa kushinda mechi hiyo Yanga wameendelea kujichimbia kileleni kwa kuwa na pointi 74 zikiwa ni pointi 17 mbele ya Yanga inapiga kimyakimya Johnson James na Leah Marco,Mwanza Simba ambao wanakamata nafasi ya tatu wakiwa na pointi 57.
Kikosi hicho kinachofundishwa na Kocha Mkongomani Mwinyi Zahera kilipata mabao yake kwa kupitia Heritier Makambo, Thabani Kamusoko pamoja na moja la kujifunga la mchezaji wa Kagera Sugar, Kassim Khamis ambaye pia alifunga bao moja la Kagera. Bao lingine lilifungwa na kiungo mkongwe Paul Ngwai Ngalyoma.
Kwa kufunga bao hilo sasa Makambo amempita mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere katika orodha ya wanaoongoza kwa kufunga mabao huku akimfukuza kinara Salim Aiyee wa Mwadui mwenye mabao 16.
Licha ya kuwafunga Kagera Sugar wanaofundishwa na kocha Mecky Maxime, Yanga watalazimika kumkosa mlinzi kiongozi Kelvin Yondani ambaye alipewa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumfanyia faulo mmoja wa wachezaji wa Kagera.
Uwanja wa Kirumba umeonekana kuwapenda zaidi Yanga kutokana na kugawa vipigo kwenye mechi zake ambazo wamecheza. Ikumbukwe kuwa waliwachapa African Lyon 2-0 kisha Kagera 3-2 katika uwanja huohuo wanaoutumia kama uwanja wao wa nyumbani kwa muda.
Stori na Johnson James na Leah Marco,Mwanza