MWANAMUZIKI wa Marekani, Kanye West, ameendelea na mpango wake wa kufanya ibada na familia yake kila Jumapili. Ibada hii hufanyika kwa burudani kubwa kutoka kwenye bendi yake Kanye West.

Ibada hiyo ambayo waumini wake hufika kwa kupewa mwaliko, si kila mtu anaweza kwenda. Unaambiwa ukipata mwaliko wa kwenda kwenye ibada hiyo unatia saini makubaliano ya kutokwenda na mtu mwengine ambaye hahusiki katika.
Wasanii ambao wamewahi kuhudhuria ibada kama hiyo ni DMX, Chance the Raper na Kid Cudi. Mke wa Kanye, Kim Kardashian, amekuwa akitumia mitandao yake ya kijamii kurusha baadhi ya picha za video kuonyesha yaliyojiri wakati wa ibada. Mara nyingi majirani zake Kanye wamekuwa wakilalamika juu ya ibada hizo anazofanya kwa kupiga kelele za muziki mkubwa nyumbani kwake au maeneo ya mlimani jirani na nyumbani kwakwe kila Jumapili.
