The House of Favourite Newspapers

MANARA AMVAA ZAHERA KUHUSU KUMTIMUA CANNAVARO

Kocha  wa Yanga, Mwinyi Zahera.

MSEMAJI wa klabu ya soka ya Simba,  Haji Manara amemjibu Kocha  wa Yanga,  Mwinyi Zahera, baada ya kumhusisha Meneja wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, na kushindwa kwa Yanga katika mechi yake ya Ligi Kuu na Simba ambapo ilifungwa bao moja na mchezaji Meddie Kagere kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Gazeti la Championi Jumatano la  Aprili 24, 2019, liliandika kwamba Zahera  alisema yeye ndiye alimtimua  ‘Cannavaro’ baada ya kuonekana kwenye ofisi ya mwekezaji wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’,  licha ya yeye (Cannavaro) kufafanua kuwa alifika katika ofisi hiyo kwa ajili ya masuala yake binafsi.

 

Manara amemjibu Zahera kupitia mtandao wa Instagram akimataka athibitishe madai yake kwamba kitendo hicho cha Cannavaro kuonekana katika ofisi hizo kililenga kuwahujumu Yanga.

Ujumbe wa Manara ni ufuatao:

Leo  ”Kwa hili Zahera hatutakubali!!
Lazma uthibitishe beyond reasonable doubt kwamba Mwenyekiti wetu wa Bodi ya Wakurugenzi alishiriki kuwahujumu Yanga Kwenye mchezo wetu na nyie!!
Kocha usiye na heshma na unaeropokwa kila siku ili utafute kiki kwa Washabiki wa Yanga!! Lazma ujue MO ni mtu mwenye heshma kubwa ktk jamii na kumhusisha na vtu vya hovyo hovyo ,Simba haitakaa kimya ( no matter TFF hawakukemei hata siku moja)
Halaf unamtaja Canavaro ili umdhalilishe,yy ndio captain bora wa muda wote Yanga kafanya mambo makubwa pale na kashinda mataji mengi mno wakati ww hata kikombe cha Uji hujashinda hapo,nia ni kutaka uwe bora kuliko uliowakuta na ambao wamefanya mambo mengi pale!!!tumekuvumilia sasa imetosha,huwezi kila siku ukaituhumu klabu yetu halaf tukukalie kimya!! Sasa utaijua ukubwa wa Simba,labda ulikuwa ukiisikia tu
Kesi hii nimeinunua kama Mkuu wa Habari wa Simba!!
Nikirudi nna ww ulete uthibitisho either TFF au Kwenye vyombo vya dola!!
Mpira hauwezi kuchezewa na watu wasiojielewa na kupayuka yuka”

Kisa Mo, Zahera Amtimua Cannavaro Yanga

Comments are closed.