MEYA wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, jana ametembelea kituo cha radio ya mtandaoni ya +255 GLOBAL RADIO na kukiri kwamba inafanya kazi katika kiwango cha hali ya juu.
Mstahiki Jacob ameyasema hayo alipotembelea ofisi za Global Group zilizoko Sinza-Mori katika kuadhimisha siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo alizungumza na kutembezwa katika idara mbalimbali zikiwa ni pamoja na kitengo cha uzalishaji Magazeti Pendwa, magazeti ya Championi na Sport Xtra, Global TV Online, na kitengo cha Teknolojia na Mawasiliano (IT).
Baada ya kutembezwa sehemu hizo, alikiri kwamba alikuwa amevutiwa na utendaji na studio za redio hiyo ambapo alisema “inaweza kuwa namba moja”.
Comments are closed.