×

Kisa ubaguzi wa rangi, Sterling apewa tuzo

MSHAMBULIAJI Raheem Sterling ametunukiwa tuzo maalum ya kuongoza kampeni ya kupinga ubaguzi wa rangi ambayo amekuwa akiifanya katika wiki za hivi karibuni. Staa huyo wa Manchester City, amepewa tuzo hiyo kutoka katika Taasisi ya BT Sport.

 

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, amekuwa akitumia ukurasa wake wa Instagram mara kadhaa akionekana kupinga wale wote wanaohusika katika ubaguzi wa watu weusi barani Ulaya.

 

Sterling alikabidhiwa tuzo hiyo huku akishuhudiwa na kocha wa timu yake ya taifa ya England, Gareth Southgate, juzi Alhamisi.

 

Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Sterling alisema alipoanzisha kampeni hiyo hakutegemea kupata tuzo bali aliifanya kama sehemu ya kufikisha ujumbe vile alivyokuwa akijisikia.