×

Video: Rais Magufuli Ashuhudia Kusimikwa Kwa Askofu Nyaisonga Mbeya


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Mkewe Janeth Magufuli  leo wameshiriki Ibada ya kumsimika Askofu Mkuu Mteule, Gervas Nyaisonga kuwa Askofu Mkuu wa kwanza  Jimbo Kuu Jipya la Mbeya.

 

Ibada inafanyika katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Rais Magufuli yupo mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi ya siku nane.

Rais Magufuli amekusanya Sadaka kwa waumini mbalimbali waliokusanyika katika ibada hiyo.

Desemba 21 mwaka jana, Papa Francis alitangaza na kumteua Askofu Nyaisonga kuwa Askofu Mkuu wa kwanza Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya na kulitangaza kuwa Jimbo Kuu teule.

Awali, Askofu Nyaisonga alikuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpanda ambaye pia ni Rais wa  Baraza la Maaskofu  Tanzania (TEC).

“TUTENDE HAKI KWA KILA BINADAMU” MAKAMU RAIS TEC