The House of Favourite Newspapers

SEKESEKE LA WANANCHI WAVAMIA MSAFARA WA HARMONIZE – PICHAZ

WANANCHI na mashabiki wa eneo la Tunduru, Barabara ya Songea, leo Jumatano mchana wamekimbilia barabarani na kuuvamia msafara wa msanii wa WCB, Harmonize aliykuwa njiani na wasanii wenzake kuelekea Siongea mkoani Ruvuma kwa ajiri ya shoo.

Mashabiki hao baada ya kuona msafara wa magari yaliyobeba wasanii na wanahabari kuelekea Songea, ghafla walijaa barabarani wakitaka kusalimiana na Harmonize hali iliyomfanya msanii huyo kusimamisha msafara na kushuka kisha kusalimiana nao na kupiga picha kabla ya kuendelea na safari yake.

Harmonize na  timu yake wanatarajiwa kufanya bonge la shoo keshokutwa, Aprili 3, 2019huko Songea.

Global TV Online itakuwa Live kukuletea shoo nzima na matukio yote yatakayojiri mwanzo hadi mwisho wa shoo hiyo.

Comments are closed.