Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni mzaazi mwenzake na msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ametikisa mitaa Mbagala jijini Dar es Salaam, leo Jumamosi, Mei 4, 2019 wakati akigawa diapers aina ya SOFTCARE kwa akina mama wa Mbagala.
Global Tv inafahamu kuwa Zari ni Balozi wa Softcare na amekuja Tanzania akitokea nyumbani kwake, Afrika Kusini kwa ajili ya shughuli za kijamii.