The House of Favourite Newspapers

UNAIBA VITI VYA KANISA? ‘SUKUMA NDANI WOTE HAWA’ – VIDEO

MKUU wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri,  ameshangazwa na watuhumiwa wakiwemo vijana na akina mama waliokamatwa kwa wizi wa vitu mbalimbali mkoani humo ukiwemo wizi wa pikipiki, viti vya kanisa, masufuria, magodoro na vyombo mbalimbali vya ndani, jambo ambalo amesema halikubaliki na wala hatoruhusu lifanyike mkoani mwake.

 

Amesema hayo wakati alipotembelea kituo kikuu cha polisi mkoani humo na kukuta watuhumiwa hao na vidhibiti vyao walivyokamatwa navyo,  hivyo kuagiza waswekwe ndani mara moja na wafikishwe mahakamani.

 

“Unakamatwa na pikipiki ya wizi Tabora? Unakuja kufanyia wizi Tabora, umechemka braza, hapa ndo umefika, hiki ni chuo kikuu, sasa nasema kamata wote hawa sukuma ndani. Unaiba mpaka viti vya kanisani? Mmeingia kwenye nyumba ya mtu mmeiba mpaka masufuria? Kamata hawa, sukuma ndani wote, kisha wapelekwe mahakamani,” amesema RC Mwanri.

SHUHUDIA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.