



Wananchi Wilayani Uyui mkoani Tabora Wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwawezesha kurasimisha mashamba yao na kupatiwa hati za haki milki za kumiliki ardhi hali inayowawezesha kujikwamua kiuchumi.
Baadhi ya wananchi hao wakizungumza wakati wa mahojiano maalum Wilayani humo akiwemo mkazi
wa Miyenze Bw. Julius Magoi amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeonesha dhamira ya dhati
kuwawezesha wananchi Vijijini kupitia Mpango wa Kurasimishaji Rasilimali na Biashara za Wanyonge
Tanzania (MKURABITA).
“ Tunamshukuru Rais Magufuli kwa kuwezesha MKURABITA kuturasimishia mashamba yetu, kuyapima
na kupatiwa hati za haki milki za kimila hali inayotuwezesha kuongeza tija katika uzalishaji mashambani
hasa katika mazao ya biashara” Alisisitiza Bw. Magoi
Akifafanua amesema kuwa MKURABITA imeendesha mafunzo yanawawezesha wakulima kuendana na
dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano kuwakwamua wananchi wanyonge hasa wanaoishi vijijini katika
Wilaya hiyo kwa kuwajengea stadi za kilimo bora, ufugaji wa kuku kibiashara, kilimo cha pamba, alizeti
na mazao mengine .
Kwa upande wake mkazi mwingine wa Kata hiyo Bi Nyamizi Shija amesema kuwa anamuomba Rais
Magufuli aendelee na jitihada zake za kuwawezesha wananchi kama ambavyo anafanya sasa kwa kuwa
wanaendelea kumuunga mkono katika kila jambo analofanya ili kuwaletea maendeleo.
Aliongeza kuwa utendaji mzuri wa Serikali ya Awamu ya Tano umewawezesha wananchi kunufaika na
rasilimali za nchi yao ikiwemo kutolewa kwa fedha zinzoelekezwa Vijijini kuwajengea uwezo akitolea
mfano urasimishaji wa ardhi ambayo ni nyenzo kuu ya kuwawezesha wananchi.
Naye mkazi wa Kata ya Lutende Bw. Omari Mohamed amesema kuwa Serikali imeonesha kuwajali,
kuwatambua, kuwathamini na kuwawezesha wananchi vijijini kwa kuwa inachukua hatua kuimarisha
sekta zenye kuwainua wananchi ikiwemo kilimo na mifugo hali itakayowezesha kufikiwa kwa malengo yakutukwamua kiuchumi kama wakulima.
“Rais Magufuli yuko makini, anatetea wanyonge na anaelewa mahitaji ya wananchi tunaoishi vijijini ndio
maana tumepata fursa ya kujengewa uwezo kupitia MKURABITA na kurasimishiwa mashamba yetu hali
iliyotuwezesha kupata hati za haki milki za kimila za kumiliki ardhi ambazo tutazitumia kujikwamua
kiuchumi” Alisisitiza Mohamed.
Akifafanua Mohamed amesema kuwa wananchi wanaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuwaletea maendeleo.
Kwa upande wake Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini kutoka MKURABITA Bw. Antony Temu amebainisha
kuwa wananchi wa Kata za Miyenze na Lutende wamejengewa uwezo wa kutekeleza kilimo chenye tija
cha mazao ya biashara kama alizeti, pamba na mengine ili waweze kuzalisha kwa tija.
Aliongeza kuwa mada nyingine walizofundishwa wakulima hao ni pamoja na utunzaji wa mazingira,
utunzaji wa kumbukumbu, fursa zilizopo katika taasisi za fedha, uandaaji wa mpango wa biashara na uanzishaji wa vyama vya ushirika.
Mafunzo ya kuwajengea uwezo wananchi waliorasimisha mashamba yao na kupatiwa hati za hakimilki
za kimila yamefanyika katika Kata ya Miyenze na Lutende Wilayani Uyui mkoani Tabora na kushirikisha wakulima zaidi ya 200.
(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)