The House of Favourite Newspapers

KISUTU, DAR: DEREVA TAKSI KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUMTEKA MO DEWJI

Dereva teksi, Mousa Twaleb (46) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumanne Mei 28, 2019 akikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kumteka mfanyabiashara, Mohamed Dewji ‘Mo’.

Twaleb wamefikishwa mahakama hapo na kusomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

 

Mo alitekwa na watu wasiojulikana alfajiri ya Oktoba 11, 2018 wakati akifanya mazoezi katika Hoteli ya Colosseum iliyopo jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, alipatikana Oktoba 20 katika eneo la Gymkhana baada ya kudaiwa kutelekezwa na watekaji hao.

 

Watu 12 walikamatwa na polisi katika tukio hilo wakihusishwa na watekaji.

Familia ya Dewji iliahidi kutoa Sh1 bilioni kwa mtu yeyote ambaye angetoa taarifa ambazo zingesaidia kupatikana kwa kijana wao. Hata hivyo hakuna aliyepata fedha hizo baada ya kupatikana kwake.

Comments are closed.