
MKURUGENZI Mtendaji (C.E.O) wa klabu ya Simba, Crescentius Magori amesema kuwa amepokea ofa nyingi kwa Meddie Kagere kuhitajika na klabu kubwa Afrika na Ulaya huku akiwataja Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Zamalek.
Kagere ni kati ya wachezaji wanaowaniwa vikali na baadhi ya klabu kubwa Afrika ikiwemo AS Vita na TP Mazembe za DR Congo zilizotangaza dau kubwa kumnasa mfungaji huyo bora wa Ligi Kuu Bara mwenye 23.
Akizungumza na Championi Jumatano, Magori alisema wamezigomea ofa hizo za njia ya simu na badala yake
kuwataka mawakala hao kufika nchini kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya uso kwa uso na siyo simu kabla ya kumuachia.
“Ukweli ni kwamba nimepokea ofa nyingi kutoka kwenye klabu kubwa Afrika na zote zikimuhitaji Kagere ambaye ndiye mchezaji tegemeo hivi sasa ndani ya Simba.
“Ofa ni nzuri za mikataba mizuri,lakini tatizo hao mawakala wanapiga simu pekee badala ya kuja nchini kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya uso kwa simu kuliko kutumia simu.
“Na sisi kama uongozi tumeachana na mawakala hao kwani sasa hivi mawakala wapo wengi wapo wajanja wajanja, hivyo kwa yule wakala anayemtaka Kagere basi waje nchini kuwaona viongozi,”alisema Magori.