×

TIMU YA SIMBA ILIVYOPOKELEWA KUTOKA MORO MPAKA KARIAKOO (PICHA +VIDEO)

KOCHA wa Simba, Patrick Aussems akishuka kwenye basi maeneo ya Kibaha, akitokea Morogoro

Wachezaji wa klabu ya Simba pamoja na mashabiki wao leo mei 29, wakitokea mkoani Morogoro wameshuka Kibaha  na kujiunga na msafara wa mashabiki wao kulinadi kombe lao kwa furaha na nderemo.

Mabingwa hao wa TPL msafara wao leo umeanzia Morogoro na walipofika Kibaha Stand wachezaji walipanda kwenye gari la wazi wakiwa na kombe lao wakiwaonyesha mashabiki ambao walijitokeza barabarani.

 

Beki wa kikosi cha Simba, Erasto Nyoni akisalimiana na mashabiki

Mashabiki wengi walijitokeza kuona namna mabingwa hao wakiwa na ubingwa wao ambao ni wa pili mfululizo kwani walitwaa pia msimu uliopita wa mwaka 2017/18.

Safari kubwa ya msafara huo iliishia makao makuu ya Simba mitaa ya Kariakoo, Msimbazi ambapo nahodha msaidizi Mohamed Tshabalala alimkabidhi kombe mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere akisalimiana na mashabiki
Mashabiki wa Simba wakiwa kwenye msafara
Kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima akisalimiana na mashabiki wa Simba
Mlinda mlango namba mbili wa Simba, Deogratius Munish akiendesha bodaboda ya shabiki wa Simba