Mastaa 15 Wasaka Timu Nyingine
WACHEZAJI 15 wa Yanga tangu jana wameanza mapambano kusaka timu mpya baada ya Mwinyi Zahera kuwachunia. Mastaa hao wengi mikataba yao imemalizika.
Zahera ameliambia Spoti Xtra kuwa, tayari ameshawaaga wachezaji hao wote ambao mikataba yao inamalizika huku akipanga kuwaita mmoja mmoja kwa ajili ya kuwasaini kwa wale atakaowahitaji pekee.
“Wapo baadhi ya wachezaji wataka-ondoka Yanga ambao wengi wao tayari wamepata timu za kwenda kuzichezea katika
msimu ujao, hivyo nimeona niwaage kabla ya mechi kwa wale nitakaowaacha kwa sababu mimi nitachelewa kurudi nchini nitakuwa kwenye Afcon,” alisema Zahera
Comments are closed.