×

Rasmi Mkude amalizana na Simba

BAADA ya kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude kuwapiga danadana za muda mrefu waajiri wake hao, rasmi ameamua kunyoosha mikono mbele ya mwekezaji wa klabu hiyo, Mohammed Dewji, kwa kuongeza mkataba wa miaka miwili.

 

Mkude ambaye msimu uliopita aliikamua Simba Sh milioni 80 kwa ajili ya kuongeza mkataba, awamu
hii tena amefanikiwa kuongeza dau lake mbele yao na kuchukua Sh milioni 100 akiwa sambamba na wachezaji wengine kama John Bocco, Aishi Manula, Erasto Nyoni na Shomari Kapombe.

Taarifa rasmi kutoka Simba imeeleza kuwa, baada ya kuwepo na mvutano wa muda mrefu baini ya uongozi wa Simba na kiungo huyo ambaye mara kadhaa alilia kuongezwa dau lake kiasi cha kutishia kusaini kwa wapinzani wao wa jadi, Yanga, wamefikia muafaka na kujizolea kitita hicho ambacho kinamfunga kuitumikia klabu hiyo
kwa misimu miwili.

 

“Simba wamempatia fedha hiyo aliyokuwa anataka na ndiyo maana amesaini miaka hiyo miwili ambayo ndiyo ilikuwa karata yake ya mwisho ya kujipatia fedha nyingi sababu baada ya miaka hiyo miwili atakuwa ametimiza miaka 30, hivyo uhakika wa kupata fedha kama hizo utakuwa ni mdogo.

 

“Lakini pia sasa mshahara wake utakuwa ni Sh milioni nane kwa mwezi badala ya Sh milioni sita alizokuwa akilipwa miaka miwili iliyopita,” kilisema chanzo hicho. Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu alipoulizwa juu ya hilo, alisema: “Kama unavyoona tunaendelea kuwatambulisha wachezaji wetu wa zamani ambao kwa jumla wameongeza mikataba.

 

“Wote ambao wameongeza tutaendelea kuwajua kadiri ambavyo taarifa za klabu zitakavyozidi kutolewa, lakini kimsingi wachezaji takribani wote waliokuwa wanamaliza mikataba yao wameshaongeza,” alisema. Alipotafutwa Mkude hakupatikana kutokana na simu yake kuita bila ya kupokelewa, ilikuwa hivyo pia kwa meneja wake