Mwenyekiti Mpya Bodi ya Airtel Atembelea Makao Makuu
Global Publishers June 14, 2019
SHARE THIS:
MWENYEKITI mpya wa bodi ya Airtel Tanzania, PLC Dkt Omary Nundu, leo Juni 14, 2019, ametembelea makao makuu ya Airtel Tanzania yaliyopo mtaa wa Morocco jijini Dar es Salaam ambapo ameahidi kushirikiana na uongozi wa kampuni hiyo kuhakikisha asilimia 49% ya hisa za kampuni hiyo zinazomilikiwa na Watanzania zinaleta tija.
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Airtel Tanzania PLC Dkt Omary Nundu (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso, leo alipotembelea makao makuu ya Airtel Tanzania yaliyopo jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mkuu mpya wa Ufundi wa Airtel Tanzania Dkt. Prosper Mafole (katikati) na Dkt Omary Nundu (kulia) wakisalimiana na Sunil Colaso.Vikao mbalimbali vilivyofanyika makao makuu leo.