×

Kahata avunja ukimya Simba

aNYOTA wa Kenya anayetajwa kuwa kwenye hatua za mwisho kujiunga na Simba, Francis Kahata amesema kila kitu juu ya hilo kitafahamika baada ya kumalizika kwa michuano  Dar es Salaam ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon).

 

Kahata anayeitumikia Kenya kwenye michuano hiyo inayoanza leo Ijumaa nchini Misri, amekuwa akihusishwa kutakiwa na Simba tangu kabla ya msimu wa 2018/19 haujaanza.

 

Kiungo huyo wa Gor Mahia amesema tayari amekutana na viongozi wa Simba na kujadili suala hilo, lakini amewasubirisha mpaka Afcon itakapomalizika. “Nina ofa nyingi, miongoni mwa hizo ni kutoka Simba.

 

Wamekuwa wakinifukuzia tangu msimu uliopita, lakini bado sijasaini kutokana na kwamba nina mkataba na Gor Mahia,” alisema Kahata.