Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, amesema kuwa laini hizo wamekuwa wakiziuza kwa wahalifu na watu wasio na vitambulisho ambao ni wahalifu.
Aidha, Muroto ameongeza kuwa wamewakamata wahamiaji haramu wanne ambao ni raia wa Ethiopia na kwamba raia hao wanne walikamatwa katika eneo la Chipolo wilayani Mpwapwa wakiwa wanasafirishwa katika basi Namba T.112 ATC, SCANIA, Bus la Kampuni ya Premiere Line linalofanya safari kutoka Mwanza kwenda Mbeya.
Muroto ameongeza kwamba kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa yote wameanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi ambavyo sasa wanalisaidia jeshi la polisi kuwaibua wahalifu wote katika mitaa yao na wapokeaji wa mali zinazotokana na uhalifu.
Aidha, amewataka madereva kuheshimu sheria za usalama barabarani na kwamba anayetembea kwa miguu ana haki ya kisheria kama dereva anaye endesha barabarani.
Naye, Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma Methew Benjamin, amesema wameamua kujikita katika utoaji wa elimu zaidi ya usalama barabarani hasa katika vivuko vya waenda kwa miguu ambapo zaidi ya asilimia 76 ya ajali za barabarani hapa nchini husababishwa na makosa ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na uzembe wa madereva.
Comments are closed.