×

Miss Universe Afunguka Alivyoifukuzia Ndoto Yake – Video

MSHINDI wa Pili wa Miss Universe Africa mwaka 2016/17, Lilian Loth, amefunguka namna alivyoanza kuitambua ndoto yake ya urembo na hatimaye kuanza kuifukuzia tangu akiwa shule ya msingi mpaka kufikia mafanikio ya juu katika tasnia hiyo.

Lillian amefunguka hayo wakati akipiga stori na Kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, saa 6:00 mchana hadi saa 10:00 jioni kupitia cha +255 Global Radio jana na kusema kuwa mtu aliyemshawishi kuingia katika urembo ni mrembo wa Kimataifa kutoka  Tanzania, Millen Magese, ambaye kwa sasa anaishi New York Marekani.

Lilian amesema  baada ya kumaliza kidato cha nne alihamia Dar es Salaam kwa ajili ya masomo Advanced Level ambapo alishiriki Miss Chang’ombe kisha Miss Temeke na kuanzia hapo nyota yake ya urembo iliwaka mpaka Miss Universe.

 

 

Lillian ambaye ni msomi wa Chuo Kikuu cha Kampala International University, hivi sasa anajishughulisha na masuala ya mitindo (Modelling).

 

Akizungumzia kuhusu wasanii wa Bongo Fleva,  Lilian amesema kuwa anampenda sana Diamond Platnumz na Vanessa Mdee kutokana na kazi zao nzuri wanazofanya.

 

Pakua App ya +255 Global Radio ili kusikiliza vipindi vyetu live, exclusive interviews, burudani ya muziki na uchambuzi wa matukio mbalimbali. BOFYA HAPA KUINSTALL APP

Tazama Interview Nzima Hapa chini