×

MSOMAJI: BETIKA LIMENITENDEA MIUJIZA

MSOMAJI wa Gazeti la Betika, Shaban Kidisa anayepatikana Mtaa wa Kongo na Pemba, Kariakoo jijini Dar es Salaam, amefichua kuwa, gazeti hilo limemtendea miujiza hadi sasa amekuwa fundi wa kubeti.

Kidisa ambaye ni mdau mkubwa wa masuala ya kubeti, amesema kuna wakati alifilisika kutokana na kuliwa sana alipokuwa akibeti, lakini kupitia maujanja ya Betika, akawa hodari.

“Gazeti la Betika limenifumbua sana kichwa changu katika masuala ya kubeti kutokana na hapo mwanzo nilifilisika kutokana na kila mara nikibeti naliwa, ikafikia hatua nikataka kumpa talaka mke wangu kutokana na kufilisika.

“Lakini nilipokuwa nalisoma Betika ambalo lilikuja kunipa maujanja ya kubeti na kushinda, nikawa siliwi tena kama zamani na sasa nimekuwa hodari wa kubeti.

“Zamani nilikuwa naenda kwenye sehemu za kubetia ndiyo nabeti huku nikiwa sina ufahamu mkubwa, lakini sasa siendi tena kwenye vibanda vya kubeti kwani Betika ni mwongozo tosha kwangu.

“Nashukuru Kampuni ya Global kwa kutuletea Gazeti la Betika kwa vijana kama sisi ambao ni wapenzi wa kubeti. Kwangu kubeti ni asili yangu na ipo kwenye damu, siwezi nikaacha,” alisema Kidisa.

Betika ambalo linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers, hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 na linaingia mtaani kila Jumatano.

Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi, mbali na kuwa na makala na odds za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi kubwa barani Ulaya.

Kila linapoingia mtaani, maofisa masoko wa Global Publishers ambayo huingia mtaani kila Jumatano wakati gazeti hilo linapoingia mtaani.

Leo Jumatano, timu ya maofisa masoko ya Global Publishers huingia mtaani kupata maoni ya wasomaji ambapo leo Jumatano ilitembelea Kariakoo jijini Dar.

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema amesema heshima ya Betika imeendelea kukua kila siku na sasa wanajivunia kuwa na idadi kubwa ya makampuni yanayotangaza biashara zao kupitia gazeti hilo hasa kwa kuwa bei yao ni nafuu na imewavutia wengi, huku akiongeza kuwa bado wanawakaribisha watu binafsi na makampuni kuleta matangazo yao.

“Hili ni gazeti la bure, linawahusu watu wazima kuanzia umri wa miaka 18, linatolewa bure kabisa kwa wauza magazeti wote nchini.

“Wanaohitaji kutangaa nasi tunapatikana kupitia namba 0755826488 na 0712595636 au barua pepe [email protected], bei zetu ni nafuu, mhusika anaweza kufika Sinza Mori, Dar, kwenye jengo letu la Global Group.”

“Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao yetu ya kijamii katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online,” alisema.