BAADA ya kupokelewa vizuri mwaka jana, mwanadada mjasiriamali, mtangazaji na msanii wa filamu Bongo, Antu Mandoza anatarajia kuja tena na urembo wa asili, Julai 27 na 28, mwaka huu akiwa na kauli mbiu; “Nywele za Asili Siyo Ushamba ni Ujanja.”

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Antu alisema tamasha hilo litafanyika ndani ya Viwanja vya Life Park, Mwenge jijini Dar.
“Mwaka jana tamasha hili lilifanyika Makumbusho na lilikuwa kubwa sana japo lilikuwa mara moja tu. Mwaka huu tena limekuja mara mbili ambapo hadi sasa muitikio ni mkubwa sana.

“Kama unajijua ni mjasiriamali wa mambo ya ngozi, nywele, ni msusi hii ni fursa kubwa sana kwako kwani siku hiyo mbali na kuuza vipodozi, wahudhuriaji watapata fursa ya kujifunza urembo wa asili kupitia kwa madaktari wetu na timu ya ushauri,” alisema Antu Mandoza.
Stori: MWANDISHI WETU, IJUMAA