×

Majembe Yanga Yaanza Kutua Dar

Wachezaji wa Yanga, Mshambuliaji Juma Balinya (Kushoto) na Beki Selemani Mustafa watua nchini kwa ajili ya kuanza kazi.

MAMBO ni motoo!!! hivi ndivyo utakavyoweza kusema ni baada ya wachezaji wa Yanga kutoka nje ya nchi wakitua nchini kwa ajili ya kuanza maandalizi Wiki ya Mwananchi na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.

Hiyo, ni baada ya jana alasiri mshambuliaji Mganda, Juma Balinya na beki wa kati Mrundi, Seleman Mustafa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa (JNIA) wa jijini Dar es Salaam.

Yanga imepanga kuanza kambi yake ya pamoja kesho Jumapili ambayo itakwenda kuwekwa Mkoani Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao na kuelekea Wiki ya Mwananchi itakayohitimishwa Julai 27, mwaka huu. Wiki hiyo ya Mwananchi, Yanga wameandaa mchezo mmoja wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Mamelodi Sundowns ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini (ABSA) utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.

 

Mwenyekiti wa timu hiyo, Dr Mshindo Msolla alithibitisha kambi hiyo kwenda kuwekwa Morogoro wikiendi hii akisema kuwa: “Maandalizi ya kambi yetu yanakwenda vizuri na wachezaji wataanza kuripoti kuanzia leo (jana).”

 

View this post on Instagram

 

from @yangasc – Hellow Wananchi,@maybinkalengo yuko tayari kwa kazi

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on