The House of Favourite Newspapers

Queen Mugase Aibuka Miss Kinondoni 2019 (Picha+Video)

USIKU wakuamkia leo yamefanyika mashindano yakumsaka mrembo wa  taji la Miss Kinondoni 2019 kwenye ukumbi wa The Life Mwenge jijini Dar es Salaam na Queen Mugese kuibuka mshindi wa Miss Kinondoni 2019 baada ya kuwazidi warembo wengine 17.

Mshindi wa nafasi ya pili ni Prisca Kisunda nafasi ya tatu ni Leila Adim nafasi ya nne Queen Anthony nafasi ya tano ilikwenda kwa Flaviana Steven.

Washindi wa nafasi tatu za juu wamepewa zawadi ambapo mshindi wa kwanza alikabidhiwa zawadi ya gari, mshindi wa pili kitanda na mshindi wa tatu alipewa TV.

Kwenye mashindano hayo jaji mkuu alikuwa ni aliyekuwa Miss Tanzania, Lilian Kamazma akisaidiwa na mwanamitindo Hamisa Mobetto, Martin Kadinda na Meneja wa vipindi +255 Global Radio, Bori Mbaraka. 

Comments are closed.