×

TIMU KUTOKA KUNDI LA TANZANIA ZATINGA FAINALI AFCON

Kikosi cha timu ya Senegal

TIMU ya Senegal na Algeria zitacheza mchezo wa Fainali ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) Cairo, Misri, Ijumaa wiki hii baada ya jana usiku kushinda mechi zao za nusu Fainali.

Senegal imeifunga Tunisia bao 1-0, Algeria iliing’oa Nigeria kwa ushindi wa mabao 2-1. Miamba hiyo ya soka ilikwenda muda wa nyongeza baada ya kutoka suluhu ndani ya dakika 90 za kawaida.

 

Timu hizi zote mbili zilikuwa kundi C ambalo lilijumuisha timu mbili za Afrika mashariki ambazo ni Tanzania na Kenya.

Senegal ilitawala mchezo kipindi cha pili ambako ilitengeneza nafasi saba kwa kupiga kiki, wakati Tunisia ilipiga mashuti mara mbili.

Katika moja ya matukio mshambuliaji nyota wa Liverpool, Sadio Mane alikosa bao akiwa katika nafasi nzuri ya kufunga.