×

Christina Shusho Atua Global, Afunguka Kuhusu Rose Muhando

Mwanamuziki wa Nyimbo za Injili Christina Shusho, akipokea Gazeti la Amani kutoka kwa  Mhariri wa Gazeti Gazeti hilo, Erick Evarist, Alipotembelea Ofisi za Global Group leo.

MWANAMUZIKI wa Nyimbo za Injili Christina Shusho leo Alhamisi 18, 2019 amefika  Ofisi za Global Group kufanya mahojiano katika kipindi Cha ‘Round About’ kinachoruka kupitia Global TV kila Jumapili.

Mtangazaji wa kipindi hicho Calvin Nyorobi akiongea na Mtandao huu wa Global Publishers amesema kuwa christina shusho amefunguka mambo mengi hususani yanayohusiana na huduma yake iliyopelekea kupata tuzo kumi na tatu kutoka Tanzania na nje ya Tanzania.

Aidha Nyorobi ametanabaisha kuwa Christina amegusia kuhusu Rose Muhando pamoja na Marehemu Ruge Mutahaba.

Usikose kutazama kipindi hicho siku ya Jumapili saa 11 jioni kupiti Global tv Online.

Subscribe hapa => GLOBAL TV ONLINE

Mhariri wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Sifael Paul (kushoto) akimkabidhi Gazeti la Ijumaa Wikienda Christina Shusho.
…Sifael Paul (kushoto)  akiongea jambo na Christina Shusho.
 Mhariri wa Gazeti la Risasi, Andrew Carlos (kushoto) akimkabidhi Gazeti la Risasi Shusho.
…Christina Shusho akisalimiana na Meneja uzalishaji wa vipindi vya +255 Global Radio, Lameck Kayamba
Calvin Nyorobi Mhariri wa habari Global TV akisalimiana na Christina Shusho