×

Mbrazili wa Simba Amkubali Mbelgiji

Beki mpya wa Simba, raia wa Brazil, Gerson Vieira Fraga.

BEKI mpya wa Simba, raia wa Brazil, Gerson Vieira Fraga, amemtaja kocha mkuu wa kikosi hicho, Patrick Aussems, kuwa ni wa kiwango cha juu.

 

Vieira amewahi kuwa nahodha wa timu ya Taifa U17 ya Brazil, iliyokuwa na wachezaji maarufu kama Neymar, Philippe Coutinho, Casemiro na golikipa Alisson Becker wa Liverpool, amesaini kandarasi ya miaka miwili ya kukipiga Msimbazi akitokea katika Klabu ya ATK FC ya India.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Vieira amesema anafurahi kuona yupo kwenye timu bora yenye wachezaji wengi wazuri wanaompa changamoto ya kupambana lakini kikubwa ni uwezo alionao kocha Aussems katika kufundisha soka.

 

“Tangu nimejiunga na Simba, najifunza vitu vingi sana, wachezaji wenzangu
walinipokea na kila mmoja yupo vizuri, na tuna kocha mwenye uwezo mkubwa.

 

Najivunia sana kuwa sehemu ya familia hii, ninatamani sana kucheza mechi yangu ya kwanza nikiwa na Simba katika Uwanja wa Taifa,” alisema Vieira. Simba bado wapo nchini Afrika Kusini wakiweka kambi katika Mji wa Rustenburg, ambapo jana jioni walikuwa Johannesburg walikocheza mchezo wa kirafiki na Orlando Pirates.

SHILOLE Amchana DIAMOND Hadharani, Aonyesha JEURI Ya PESA Kwa WAANDISHI!