×

EXCLUSIVE INTERVIEW Kuelekea Siku ya MWANANCHI YANGA SC

Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Siku ya wananchi ya klabu ya Yanga amewataka wanachama wa Timu hiyo nchini kujitokeza kwa wingi katika Siku ya kilele Cha Mwananchi.

Akizungumza na Global TV David Ruhago amesema Kila kitu kinaenda vizuri Kama ilivyo pangwa na tayari baadhi ya vikundi Mbalimbali vya hamasa vinaendelea kufanya Shughuli za kijamii.

Hata hivyo Ruhago amesema kuwa Siku ya kilele Cha mwananchi ambayo watacheza na Kariobang Shaki kutoka Kenya na kutangaza mfumo mpya wa kuandikisha mashabiki wao kwa njia ya App.

Siku ya Mwananchi inatarajiwa kufikiwa kilele Agast 10 mwaka huu kwa kucheza dhidi ya Kariobangi Shaki ya Nchini Kenya.