×

Ulevi Wamponza Alicia Fox, Atimuliwa Mashindano

STAA wa kike wa mieleka, Alicia Fox inasemekana alitimuliwa kutoka katika mashindano ya SummerSlam hivi karibuni kutokana na kosa la kugombana na shabiki na kibaya zaidi alikuwa amelewa chakali.

 

Fox alikuwa amerudishwa kwenye gemu baada ya kuwa amesimamishwa kwa kosa la kugombana na mume wa staa mwenzake wa mieleka, Ronda Rousey.

 

Kufuatia kosa hilo la kukorofishana na Travis Browne, ambaye ni mume wa Rousey, alitimuliwa katika mashindano ya mieleka ya Wrestlemania 34.

 

Wakati anagombana na mume wa Rousey inadaiwa pia kuwa Fox alikuwa amelewa. Hata hivyo, kufuatia kosa hilo lilifanya mdau wa Kampuni ya Kuandaa Mapambano ya Mieleka Marekani (WWE), Arn Anderson kutimuliwa kutoka katika kazi yake kwa kumruhusu Fox kuingia eneo la mchezo akiwa amelewa.

 

WWE inadaiwa kuwa ilimtaka Fox ajiunge na kliniki za kutoa ushauri nasaha ili aachane na masuala ya pombe lakini amegoma.

FULL VIDEO: MKUTANO WA SADC ULIVYOFUNGWA” Tupambane dhidi ya Ugaidi”