Jumanne Wilson, mkazi wa jijini Dar es salaam, anamlilia Rais Dk. John Pombe Magufuli amsadie kukamatwa kwa mtu aliyejitambulisha kama ni askari Magereza ambaye anamtuhumu kumpiga, kumjeruhi vibaya na kusababisha kifo cha mwanae ALOYCE WILSON, aliyefariki dunia Jumatatu ya Agosti 12, 2019. Licha ya picha za CCTV Camera kuonesha tukio zima, akiwemo mtuhumiwa, lakini polisi hawajamkamata!