
MASHABIKI wa Rais Donald Trump wa Marekani, wamemwashia moto rapa ASAP Rocky kwa kutomshukuru rais huyo baada ya kumsaidia kwenye kesi yake nchini Sweden.
.
Rocky aliwashukuru watu wote waliomsaidia lakini hakumtaja Trump wala watu wake moja kwa moja, jambo ambalo limewafanya wafuasi wa Trump kumjia juu, wakimwita mtu asiye na shukurani kwa madai kuwa alishindwa hata kumpigia simu kumshukuru.


Rais Trump alishiriki kwa kiasi kikubwa hadi rapa huyo akaachiwa huru kutoka kwenye gereza nchini Sweden ambapo alikuwa anashikiliwa kwa mwezi mzima baada ya tukio lake la kumpiga na kumshambulia raia wa nchini humo.