MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, leo Agosti 30, 2019, amekutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Sudan, IGP Adil Mohamed Ahmed jijini Dar es Salaam.
IGP Ahmed yuko nchini hapa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ya kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya majeshi ya polisi ya Tanzania na Sudan.
Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Sudan, Adil Mohamed Ahmed (kushoto), akisaini kwenye kitabu cha wageni alipowasili makao makuu ya Jeshi la Polisi nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili iliyolenga kuimarisha ushirikiano uliopo kati majeshi ya polisi ya Tanzania na Sudan. IGP Ahmed akizungumza na makamishna na maofisa wakuu waandamizi wa jeshi la polisi nchini (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam.…Akimpa zawadi IGP Sirro.IGP Ahmed na IGP Sirro wakiwa na makamishna na maofisa wakuu waandamizi baada ya kumaliza kikao kilichofanyika makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam.